Katika operesheni ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya (DCEA) Kanda ya kaskazini wamefanikiwa kuteketeza zaidi ya ekari 50 za bangi eneo la kisimiri wilayani Arumeru, ambazo zilikuwa zimepandwa kwa kuchanganywa na mazao mengine ya chakula kama mahindi, maharage na alizeti.
Akizungumza wakati wa zoezi la kufyeka na kuchoma moto likiendelea mkuu wa operesheni-DCEA Kanda ya Kaskazini Innocent Masangula ameeleza kuwa wakifanya makadirio ni zaidi ya guni 350 za bangi wameteketeza kwenye mashamba hayo.
Kwa upande wake Shabani Miraji, Afisa Elimu Jamii DCEA Kanda ya Kaskazini licha ya kuwakumbusha madhara ya dawa hizo amesisitiza namna kilimo hicho kinavyohatarisha usalama wa mazao ya chakula.
Naye Afisa Sheria wa Mamlaka hiyo Benson Mwaitenda ameeleza adhabu zinazowakabili wanaojihusisha na biashara na ulimaji wa dawa za kulevya ikiwemo kifungo cha miaka 30 au maisha jela.