Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imetoa wito kwa wananchi na makampuni kujisajili na kuongeza matumizi ya bima katika sekta mbalimbali ili kurahisisha na kupunguza gharama za juu zilizopo katika huduma zitolewazo katika Jamii.
Meneja wa (TIRA) Kanda ya Mashariki Frank Fred Shangali ametoa wito huyo katika maonyesho ya 47 ya biashara Sabasaba katika Banda la Kijiji cha Bima jijini Dar es Salaam ambapo ameongeza kuwa jumla ya Makampuni 33 wameshirikiana nao katika utoaji wa leseni wa bidhaa zipatikanazo katika huduma za bima nchini.