Nchini Burkina Faso, shirika la kitaifa linalopambana dhidi ya makosa ya Ulaghai (CNLF) limetangaza siku ya jumatatu kwamba limekamata zaidi ya tani kumi za kuku wasiofaa kuliwa, waliotokea Ulaya na kuingizwa kinyume cha sheria nchini Burkina Faso.
Kulingana na Yves Kafando, mratibu wa kitaifa wa CNLF, kuku hawa walikusudiwa kuuzwa kwa wakazi. Lakini matumizi yao yanaweza kuwa hatari sana kwa afya.
Hali za usafiri hazijazingatiwa, na ni bidhaa ambazo ziliwekwa kwenye friji muda mrefu na zilipaswa ziagizwe chini ya hali ya joto fulani, ambazo kwa bahati mbaya zimefungwa kwenye magari ambayo hayafai kwa aina hii ya usafiri.
Na tulipata kifurushi ambacho kilikuwa kimechanika tulikuta baadhi ya kuku wameanza kuyeyuka kwa hivyo kulikuwa na maji yanayotoka.
Baadhi ya bidhaa hazikua katika mazingira mazuri”.
Anaongeza: “Lazima isemwe kwamba hii inaleta tatizo la usafi wa afya ya umma na haiwezi kubaki hivyo bila kusababisha madhara kwa afya ya binadamu.
Kwa muda mrefu, mtu anaweza kupata magonjwa ambayo yanaweza kuwa mfululizo kwa matumizi ya aina hii ya bidhaa lakini hatua yetu ya leo inalenga kulinda raia, kulinda wanunuzi na kwa kweli tuna kazi ngumu ya kuweza kusambaratisha mitandao mbalimbali inayoendelea kama hii”
Yves Kafando pia anabainisha kuwa madereva saba walikamatwa huku wengine sita wakiwa mafichoni na hawakuweza kutambuliwa.