Mamlaka za Palestina katika Ukanda wa Gaza zimeurejeshea utawala wa Israel kontena lililobeba miili ya Wapalestina 88 ambayo haitambuliki kutokana na kutoambatanishwa na taarifa zozote kuhusu utambulisho wao.
Dr. Ismail Al-Thawabta, Mkurugenzi wa Ofisi ya Habari ya Serikali ya Palestina katika Ukanda wa Ghaza, amesema miili hiyo ilikabidhiwa na Israel huko kusini mwa ukanda huo ikiwa imetiwa kwenye kontena bila kufanyika uratibu wowote na Wapalestina au taasisi za kimataifa.
Dokta Thawabtah amefafanua kwa kusema: “imetolewa kwa njia ya kiburi na udhalilishaji ambayo inayoonyesha dharau kwa utu wa Mashahidi. Hiki ni kitendo kisicho cha kibinadamu”.
Ameongezea kwa kusema, Serikali ya Palestina katika Ukanda wa Ghaza imeamua kuirudisha miili hiyo kwa Israel hadi taarifa na nyaraka zinazohusiana nayo zitakapotolewa”.
Thawabtah amelaani kitendo hicho cha utawala wa Israel akikielezea kuwa ni “jinai inayochukiza inayokiuka sheria za kimataifa na sheria za kibinadamu