Mumiliki wa kundi la mamluki la Wagner, ametishia kuwaondoa wapiganaji wake kutoka mji wa Bakhmut, Ukraine wiki ijayo, akilishutumu jeshi la Russia kwa kukosa kuwapatia risasi wapiganaji wake na kupelekea kupoteza wapiganaji kadhaa.
Yevgeny Prigozhin, mfanyabiashara tajiri mwenye mahusiano ya muda mrefu na rais wa Russia Vladimir Putin, amedai kwamba wapiganaji wa Wagner wamekuwa wamepanga kuudhibithi mji wa Bakhmut ifikapo May 9, siku ambayo ni muhimu sana kwenye kalenda ya Russia kuadhimisha kushindwa kwa wanazi wa Ujerumani, wakati wa vita vya pili vya dunia.
Prigozhin amesema kwamba hawajapokea risasi za kutosha kutoka kwa jeshi la Russia tnagu jJumatatu.
Prigozhin anajulikana kutoa madai bila ushahidi wowote pamoja na vitisho ambavyo hatimizi.
Saa chache kabla ya kutoa taarifa yake, msemaji wake alichapisha video inyoonyesha akiwa mwenye hasira, akimtaka waziri wa ulinzi wa Russia Sergei Shoigu, na mkuu wa jeshi Valery Gerasimov, kumpa risasi.