Manchester United na Manchester City wanamtolea macho mshambuliaji wa Sporting CP Viktor Gyokers.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uswidi anatarajiwa kuondoka Sporting msimu huu wa joto, huku mkataba wake ukiwa na kipengele cha kununua cha pauni milioni 65.
Kocha wa zamani wa Sporting Ruben Amorim ana nia ya kumleta Gyokeres Uingereza na Old Trafford.
Lakini gazeti la The Sun linasema City pia wanavutiwa, ambapo mkuu wa michezo wa Sporting Hugo Viana atachukua usukani mwaka ujao.
Kwa kipengele cha ununuzi, uamuzi wa mwisho utaachwa kwa Gyokeres iwapo klabu zote za Manchester zitafikia bei