Manchester United wana matumaini ya kukubaliana mkataba mpya na nahodha Bruno Fernandes.
Mkataba wa sasa wa kiungo huyo unatarajiwa kumalizika msimu wa joto wa 2026 na United wanataka kukubaliana masharti mapya.
Fernandes amekuwa Old Trafford tangu 2020 na kuwa sehemu muhimu ya timu wakati huo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alifanywa nahodha wa klabu na meneja Erik ten Hag mnamo 2023 na alifunga mabao 15 katika mechi 48 katika mashindano yote msimu uliopita.
Fernandes alihusishwa na kuondoka United mapema msimu huu wa joto, lakini alifichua mwezi Mei kwamba alikuwa na nia ya kusalia ikiwa matarajio yake yatatimizwa.