Manchester United wanaongoza katika kinyang’anyiro cha kuwania saini ya beki wa Bayern Munich Matthijs de Ligt, 24.
Kulingana na ripoti ya Uhamisho wa Soka, Manchester United wanataka kuimarisha safu yao ya ulinzi katika siku za usoni, na Mashetani Wekundu macho yao yameelekezwa kwa Matthijs de Ligt.
Beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 24 hajatulia katika klabu ya Bayern Munich na anaweza kutafuta kuhama msimu wa joto.
De Ligt alikuwa tayari nyota wakati wa ujana wake, kwani mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi aliiongoza klabu yake ya utotoni Ajax hadi nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa akiwa na umri wa miaka 19 tu. Ilikuwa ni timu iliyojaa mastaa wajao, na alikuwa kiongozi wao.
Tayari wamewasiliana na wawakilishi wa Mholanzi huyo mara kadhaa,walijaribu hata kumsajili tena mnamo 2019 kabla ya kujiunga na Juventus.