Viongozi wa Manchester United wamesafiri hadi Getafe kujadili mustakabali wa Mason Greenwood, kulingana na Marca.
Greenwood, ambaye yuko kwa mkopo wa msimu mzima huko Getafe, ana mkataba na United hadi Juni 2025.
Mshambulizi huyo wa Uingereza ameonyesha kiwango kizuri nchini Hispania, akifunga mabao manane na kutengeneza mengine matano katika mechi 26 kwenye michuano yote akiwa na kikosi cha Madrid.
Getafe wana nia ya kuongeza mkopo wa Greenwood kwa msimu zaidi huku vilabu vingine, vikiwemo Barcelona na Atletico Madrid, vimeonyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22.