Manchester United wanaweza kumnunua Kylian Mbappe ikiwa unyakuzi wa Sheikh Jassim bin Hamad Al Thani utakamilika kama ilivyotarajiwa.
Inadaiwa Sheikh Jassim ameshinda kinyang’anyiro cha kukamilisha ununuzi wa Mashetani Wekundu kwa pauni bilioni 6.
Tajiri huyo wa Qatar anafikiriwa kusimamisha ushindani kutoka kwa mkuu wa INEOS Sir Jim Ratcliffe, miezi tisa baada ya Glazers kuuza klabu hiyo ya Ligi Kuu.
Sheikh Jassim anatazamiwa kukamilisha unyakuzi wake mwezi Oktoba, jambo ambalo linaondoa uwezekano wa United kumsajili Mbappe kabla ya dirisha la usajili linaloendelea kufungwa Septemba 1.
Hata hivyo mshindi huyo wa Kombe la Dunia mwenye umri wa miaka 24 anaweza kunyakuliwa ndani ya mwaka mmoja. .
Mbappe anataka kuondoka Paris Saint-Germain mkataba wake utakapokamilika msimu ujao wa joto, huku Real Madrid wakiongoza katika mbio za kuwania saini yake.
Hata hivyo PSG wamedhamiria kumsainisha mkataba mpya ili kumzuia kuondoka katika mji mkuu wa Ufaransa kwa uhamisho wa bure.