Kovacic, 29, ametia saini mkataba wa miaka minne na mabingwa hao wa Ulaya ikiwa ni usajili wa kwanza wa Pep Guardiola msimu wa joto – ikiwa ni zaidi ya wiki mbili tangu kushinda mataji matatu.
Lakini, licha ya mafanikio yao msimu uliopita, City hawana hali ya kupumzika na wamefanya haraka kufuatia kuondoka kwa Ilkay Gundogan.
Mjerumani huyo ambaye alifunga katika fainali ya Kombe la FA dhidi ya Manchester United mapema mwezi huu, amejiunga na Barcelona kwa uhamisho wa bure baada ya miaka saba kwenye Uwanja wa Etihad. City wamekuwa wakihusishwa na viungo wengine, akiwemo Declan Rice, msimu huu wa joto, lakini Kovacic amekuwa wa kwanza kupitia mlangoni.
City watailipa Chelsea takriban pauni milioni 34 kwa ajili ya kumnunua Kovacic, ambaye alikuwa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake wa miaka mitano Stamford Bridge kufuatia uhamisho wake kutoka Real Madrid.
Awali Kovacic alijiunga na The Blues kwa mkopo wa msimu mzima lakini akafanya uhamisho huo kuwa wa kudumu baada ya kufanya vyema katika kampeni za 2018/19.