Meneja wa Manchester United Erik ten Hag ana wasiwasi kuwa timu yake “haiko tayari” kwa mechi ya kwanza ya Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Fulham siku ya Ijumaa.
Wachezaji wapya waliosajiliwa Matthijs de Ligt na Noussair Mazraoui watakuwa kwenye kikosi hicho lakini waliwasili Alhamisi.
Wamekuwa na nafasi finyu ya kufanya mazoezi na wenzao wapya, na kumwacha meneja Ten Hag na kizungumkuti cha kuchagua wachezaji 11 wa kwanza watakaomenyana na Fulham Old Trafford.
Wakati huohuo, beki Luke Shaw anauguza jeraha la mguu huku naye mlinzi mpya aliyenunuliwa kwa dau la £52m Leny Yoro akipata jeraha litakalomuweka nje kwa miezi mitatu naye fowadi Rasmus Hojlund pia akiguza jeraha la paja.
United ilijitolea kutumia karibu pauni milioni 60 kuwaleta mabeki De Ligt na Mazraoui kwenye klabu kutoka Bayern Munich.“Timu haiko tayari lakini ligi inaanza,” alisema Ten Hag.
“Kuna mameneja wengi zaidi ambao wanakabiliwa na tatizo hili lakini inabidi tuanze.”Hatuwezi kujificha. Hatuwezi kuikimbia. Tunapaswa kukabiliana nayo.