Imekuwa ni kawaida kwa vilabu vya soka vya Ulaya ila mwaka kubadili aina ya jezi kwa ajili ya msimu mpya, lengo kubwa la kubadili aina ya jezi huwa inatajwa kuwa ni namna ya kutengeneza mauzo ya jezi na kuongezea mapato kwa klabu. January 5 footy headlines imetangaza kuvuja kwa aina ya jezi za ugenini watakazo vaa klabu ya Manchester City kwa msimu wa 2016/2017.
Jezi hizo mpya za Man City zinatajwa kuvuja na zitakuwa na rangi ya machungwa na zikichanganyika na rangi ya zambalau, hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Man City kuvaa jezi zenye rangi ya machungwa kwa mechi za ugenini toka wafanye hivyo msimu wa 2008/2009.
Jezi hizo mpya ambazo zitakuwa za tatu kwa Man City zinatajwa kuzinduliwa mwezi September, lakini bado hawajaonesha rasmi picha ya jezi hizo zaidi ya kuvuja kwa Logo na Nike na Etihad wataendelea kuwa wadhamini wa Man City kama kawaida. Rangi ya jezi hizo inatajwa kuja kuwashangaza wengi kutokana na uwepo wa rangi ya machungwa ambayo mara ya mwisho kuvaliwa ilikuwa miaka nane nyuma.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.