Ni Agosti 19 ,2023 ambapo Kocha wa Klabu ya Young Africans, Miguel Gamondi amezungumza na vyombo vya habari kuhusu kuelekea mchezo wa Yanga DC dhidi ya ASAS Djibouti FC utakaochezwa kesho kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi Jijini Dar es Salaam.
“Kitu muhimu zaidi kwenye mchezo ni kufunga magoli, tumejiandaa na tumelifanyia kazi hilo na ninaamini kesho mtaona mabadiliko makubwa kwenye eneo hilo” – Kocha wa Klabu ya Young Africans SC, Miguel Gamondi
“Tunakwenda kuiwakilisha Yanga na Tanzania kwa ujumla, naamini kesho tutakuwa na mchezo mzuri na kuwa na mwanzo mzuri kwenye Ligi ya Mabingwa”- Kocha wa Klabu ya Young Africans SC, Miguel Gamondi