Mbunge Mteule Viti maalumu Mkoa wa Kagera Regina Zachwa ameshiriki katika kampeni za kumnadi mgombea Ubunge Jimbo la Bukoba Mjini Adv. Stephen Byabato Sanjali na kuomba kura za Mgombea Urais CCM Dkt. Magufuli na Madiwni.
Kampeni hizo zimefanyika katika kata ya Nyakanyasi Jimbo la Bukoba Mjini Regina amewataka WanaCCM na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kupiga kura October 28 na kukichagua Chama cha Mapinduzi.
Nae Mgombea Ubunge (CCM) Bukoba Mjini Adv. Stephen Byabato amesema anafahamu vyema changamoto zinazowakabili wananchi wa Jimbo hilo hasa katika sekta ya Afya, Elimu, Miundombinu ya barabara hivyo amewataka wananchi wampe ridhaa ya kuwaongoza ili akatatue changamoto hizo.