Mechi za Ligi Kuu Uingereza zimeendelea usiku wa January 12, kwa klabu vya Machester United kuwa mgeni wa Newcastle United katika dimba la St James’ Park, wakati Bournemouth walikuwa wenyeji wa West Ham United na Aston Villa wenyeji wa Crystal Palace.
Mchezo wa Man United ndio mchezo ambao ulikuwa unapewa nafasi kubwa ya kutazamwa na watu wengi zaidi, kwani timu hiyo ina wapenzi wengi na kocha wake Louis van Gaal amekuwa kwenye headlines za kuhusishwa kufukuzwa kila siku kutokana uongozi kudaiwa kutoridhishwa na kiwango cha timu yake.
Mchezo huo ulimalizika kwa Newcastle United kutoka sare ya goli 3-3 na Man United katika uwanja wake wa nyumbani, hayo yalikuwa matokeo ambayo yaliwashangaza wengi, hususani mashabiki wa Man United, kwani hadi dakika ya 89 walikuwa mbele kwa goli 3-2, hivyo goli la dakika ya 90 la Paul Dummett lilivunja nguvu na kuishangaza Man United.
Magoli ya Man United yalifungwa na Wayne Rooney kwa mkaju wa penati dakika ya 9, na dakika ya 79 akafunga goli la tatu, baada ya Jesse Lingard kupachika goli la pili kwa Man United dakika ya 38. Magoli ya kusawazisha ya Newcastle United yalifungwa na Georginio Wijnaldum dakika ya 42, Aleksandar Mitrovic dakika ya 67 na Paul Dummett dakika ya 90, nakufanya Man United iliyokuwa na matumaini ya kuvuna point zote tatu hadi dakika ya 89, kuambulia point moja pekee.
Video ya magoli ya Newcastle United Vs Man United
https://youtu.be/-TOx3ZNiVtU
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.