Ikiwa zimepita siku kadhaa tu toka Ligi Kuu mbalimbali barani Ulaya zianze August 18 imepigwa michezo kadhaa ya kutafuta nafasi ya kufuzu kucheza katika hatua ya makundi ya Kombe la klabu bingwa barani Ulaya, michezo iliochezwa ni pamoja na mchezo ambao umewakutanisha Manchester United dhidi ya Club Brugge ya Ubelgiji.
Mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa nyumbani wa klabu ya Club Brugge nchini Ubelgiji katika uwanja wa Jan Breydel wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 29,472, mchezo umemalizika kwa klabu ya Manchester United kuibuka na ushindi wa jumla ya goli 3-1 magoli ya Man United yakifungwa na Mephis Depay dakika ya 13 na 43 kipindi cha kwanza kabla ya goli la tatu kufungwa na Marouane Fellaini dakika ya 90 ya mchezo goli la kufutia machozi kwa klabu ya Club Brugge lilifungwa dakika ya 8 kwa Michael Carrick kujifunga.
Hii ni video ya magoli mtu wangu
https://youtu.be/ZSCeGVOhzFc
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos