Wananchi wa kata Ayalagaya Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara wameamua kuipandisha hadhi Zahanati ya kijiji cha Dereda kati kwa kujitolea nguvu kazi ikiwa ni pamoja na Uchimbaji wa Msingi kwaajili ya kukamilisha Majengo yatakayoishawishi Wizara ya Afya nakuwa kituo cha Afya.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Bw, Madama Hosea amesema tayari mchakato wa kuipandisha Zahanati hiyo kuwa kituo cha Afya tayari umeanza pamoja na kuongeza watumishi ili kuondoa changamoto wanazokutana nazo wakinamama kufuata huduma za Afya kwa umbali wa zaidi ya Kilometa 10.
Nae Mkurugenzi wa Shirika la Karim Foundatio Bw, Shau Erro amesema wamekuwa wakiisaidia Jamii katika masuala mbalimbali ikiwemo Afya pamoja na Elimu ambapo jengo hilo litagharimu zaidi ya shilingi Milioni 132 na litakamilika ndani ya miezi minne hivyo ameiomba serikali kupeleka vifaa ili Wananchi kupata huduma zilizokusudiwa.