Katika kuendelea kudumisha amani Upendo, na Utulivu wa nchi,huduma ya uamusho na matengenezo ya kanisa ulimwenguni imeandaa kongamano la kimataifa la kuombea Taifa la Tanzania na viongozi katika ngazi zote ili waendelee kuongoza katika njia njema na kuweza kutimiza kusudi walilopewa.
Akizungumza na waandishi wa habari Leo Jijini Dar es salaam Mwalimu wa neno la Mungu kutoka katika huduma hiyo AUGUSTINE TENGWA amesema kongamano Hilo litafanyika April 28 siku ya Jumapili katika katika viwanja vya Suma Jkt MWENGE huku akiwakaribisha watu wa dini zote kushiriki maombi hayo ambayo yataleta Tija Kwa Taifa.
Aidha amesema ni wakati muafaka Sasa kama watanzania kusimama imara kuliombea Taifa na viongozi wanaliongoza Ili liendelee kuwa katika amani na Utulivu na kukuza uchumi.
Akieleza kuhusu Mvua zinazoendelea hivi Sasa Mtumishi TENGWA ameitaka jamii kutokusema kuwa Mvua hizo ni laana Bali ni Baraka kutoka Kwa Mungu na kwamba zaidi ya yote yanahitajika maombi Ili zisizidi kuleta maafa zaidi