Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji wa Kibiashara wa Ng’ombe(TCCS)Naweed Mulla wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya maonesho ya mifugo na mnada unaotrajia kufanyika Juni 14 -15,2024 maeneo ya Ubena Estate Chalinze.
Alisema lengo la kuanzisha programu hizo ni kusaidia wakulima na wafugaji kujikwamua kiuchumi wao wenyewe na kuongeza pato la taifa kupitia ufugaji.
Alisema takribani washiriki 300 ,wanatarajia kuhudhuria maonesho hayo ambayo yatafanyika ndani ya siku tatu katika viwanja hivyo,yakiwa na lengo la kuwawezesha wafugaji,wasindikaji na wadau mbalimbali nchini kushawishi sera za maendeleo na kukuza uzalishaji wa mifugo endelevu kwa njia ya kuwajengea uwezo na mitandao.
Alisema maonesho hayo yanania ya kuwezesha Jukwaa Madhubuti la Kitaifa la Wafugaji ,wasindikaji na wadau katika mnyororo wa thamani ya mifugo kutambulika kwa lengo moja la kuendeleza sekta hiyo kwa mbinu bora endelevu za kiuchumi na kimazingira.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugezi Idara ya Mipango,Ushauri na Mahusiano ya Taasisi wa Benki ya Kilimo,Mkani Waziri alisema wao kama benki kazi yao kubwa na kutoa maendeleo katika sekta ya kilimo,mifugo na uvuvi hivyo wameamua kushirikiana na TCCS kuona namna wanavyoweza kuleta mageuzi katika tasnia ya ufugaji.
Alisema wamekuwa washiriki wakuu katika tasnia ya ufugaji ili kuhakikisha watanzania wanafuga kwa tija na kuweza kupata kipato cha kugeuza maisha yao .”Tunatoa mikopo ya moja kwa moja kwa wafugaji katika kuwawezesha wafugaji ambapo hadi sasa benki imetoa jumla ya Bilioni 38 ya mikopo kwa wafugaji kwa wanufaika wapatao 8688 katika mikoa 21,”alisema na kuongeza
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Mkoani Pwani, Ngobere Msamau alisema kupitia maonesho hayo wanatarajia kupata elimu ya kufanya wazidi kuongeza tija katika ufugaji wa kisasa na kuondokana na ule wa kienyeji.
”Maonesho haya yanatupa kujifunza mambo mbalimbali ya ufugaji wa tija na waasili na kuona namna gani wenzetu walivyopiga hatua katika ufugaji bora,”alisema.