Ni Julai 12, 2023, Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Jerry Silaa ambae amekutana na Vyombo vya Habari kuhusu suala la Uwekezaji wa Bandari.
“Wiki iliyopita serikali iliingia mkataba na Uropean Union ya Budget Support, mliona watu wakijadili kuwa fedha hizi zinatoka kwa Mzungu? Juzi tumepitisha bungeni bajeti ya Sh Trilioni 44.39. Lakini watu wameshika jambo moja tu, hivyo nashawishika kusema kuwa kuna nguvu inatumika nyuma ya hawa wanaopotosha. Ndio maana nimeona nije hapa kutoa wito kwa serikali juu ya suala hili la bandari,”Jerry Silaa Mbunge Ukonga.
“Jamii ya Kitanzania ni watu wenye busara na kuheshimiana sana na watu wanaojadiliana mambo kwa hoja. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) tulipata maoni mengi kutoka kwa Watanzania na wasomi wengi. Maoni mengi yanahusika zaidi na mikataba ya utekelezaji na yamepelekwa serikalini yazingatiwe kwenye uaandaaji wa mikataba hiyo. Na Mheshimiwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema maeneo yote hayo yatazingatiwa.” Jerry Silaa Mbunge Ukonga.