Halmashauri ya Mji wa Geita kwa klushirikiana na wadau wa Maendeleo Nchni kupitia Taasisi ya African Creative inayofanya kazi ya usafi wa Mazingira katika Mgodi wa Geita Gold Mining imeandaa Maonyesho ya wajasiliamari wadogo wakiwemo wafugaji,wavuvi na wakulima yanayotarajiwa kufanyika Mei 26 mwaka huu Mkoani Geita.
Akizungumza katika Mkutano na wandishi wa habari Makao Makuu ya Taasisi hiyo Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Geita Bi.Zahara Michuzi amesema kwa upande wa kilimo tayari serikali imetenga eneo la Ibanda Irigation Skimu pamoja na fedha shilingi Bilioni 5.6 kwa ajili ya kutatua changamoto za kilimo ndani ya Halmashauri ya Mji wa Geita.
“Kwa kuunga mkono Serikali ya awamu ya sita Halmashauri ya Mji wa Geita tayari tumeanza kuopareti machinjio yetu ya Mpomvu ya Kısasa kuhakikisha kwamba Bidhaa zote za Nyama zinatoka kwa bora tukishirikiana na mwengangu wa SIDO kutoa mafunzo ya Namna gani ya Kupakeji kuchinja kuandaa hata ile mboga ili iweze kushindana katika Masoko ya ndani na Nje ya Nchi sambamba na hilo katika suala la kilimo tumetenga eneo la ibanda skimu ambapo ishatengewa Bilioni 6.5 mwaka wa fedha 2022/2023 na mradi upo katika hatua ya upembuzi yakinifu,” Mkurugenzi Halmashauri Mji Geita.
Michuzi amesema tayari wameimaimarisha ulinzi na usalama huku akiwataka wakazi wa Mkoa wa Geita na wageni kutoka maeneo mengine ya Mikoa ya Tanzania.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya African Creative na Mwenyekiti wa kamati ya Maonyesho ya 4 ya Fahari Geita Ndg.Raphael Siyantemi amesema maonyesho hayo yanatarajiwa kufunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigella yatakayohusisha washiriki wapatao 260 na wadau 56 kutoka serikalini na Sekta Binafsi.
Naye Meneja wa SIDO Mkoa wa Geita Bi.Nina Nchimbi amesema wanashirikina na wadau wa Sekta Binafsi katika kuhakikisha kila mkulima,Mvuvi,Mfugaji wanapata Fursa ya Kutosha katika kuonyesha Mazao .
Bi.Nchimbi ameendelea kusema kuwa wanafanya jitihada za kuongeza thamani ya Mazao kupitia wajasiliamari mbalimbali wakiwemo wakulima,wafugaji na wavuvi ndani ya Mkoa wa Geita katika kuunga Mkono Jitihada za Serikali ya awamu ya Sita Chini Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kuwakwamua wajasiliamari.