Moja ya kisa kilichoishangaza dunia ni pamoja na simuzi ya mabinti mapacha wenye umri wa miaka 22 walioungana viungo vyao vya mwili waliojulikana kwa majina ya Carmen na Lupita Andrade. Zaidi ya fact ya kuwa wawili hao wameungana, kilichoteka maskio na macho ya watu wengi ni mabinti hao kufunguka kuhusu uzoefu wao wa kushare boyfriend mmoja katika mahojiano na kituo cha tovuti ya “Today.com”
Carmen na Lupita walihamia nchini Marekani kutokea Mexico walipokuwa watoto wachanga, ingawa wanaelewana sana walikubali kwamba kila siku huwa ni njema kwao wakiwa wanaelewana ila walibainisha kuwa mara nyingi hisia za kila mmoja hutiliwa maanani. “Ninaweza kuhisi wakati Carmen ana wasiwasi au karibu kulia,” Lupita alisema. “Ni tone moja la tumbo.” Walibainisha kwamba ikiwa wangefanyiwa upasuaji wa kutengana, mmoja wao au wote wawili wanaweza kufa kwa sababu wanashiriki viungo vya ndani.
Katika mahojiano yao, mabinti hao wawili walielezea ugumu wa mmoja wao kuwa na boyfriend licha ya kushare viungo vya mwili hususani sehemu zao za siri, mfumo wa uzazi na hata mzunguko wa damu. Kila mmoja wao anaseti ya mikono lakini kila mmoja anacontro mguu mmoja tu. Lupita anasema kwamba yeye hayupo kwenye mahusiano lakini hataki hilo limzuie dada yake Carmen kuwa boyfriend na hatimaye kutulia na kuanzisha familia.
Carmen alisema alikutana mpenzi wake Daniel kwa njia ya mtandao mnamo Oktoba 2020, hakuwahi kujaribu kuficha ukweli wa kwamba yeye na pacha wake wameungana, kwahiyo alipata messages nyingi kutoka kwa wanaume wengi kutokana na utofauti wa story yake. Kilichomvutia kutoka kwa boyfriend wake ni kwasabau hakumuuliza maswali mengi alimchukulia jinsi alivyo.
Carmen na Daniel wapo pamoja kwa zaidi ya miaka miwili sasa na Carmen alisema kwamba kuna wakati fulani huwa anajiskia vibaya kutokana na kutaka kuspend muda mrefu na mpenzi wake hivyo mara nyingi humruhusu dada yake kuchagua mahali watakapoenda kula chakula cha jioni iliasijiskie vibaya.
Dada hao wamekuwa kwenye mitandao ya kijamii kwa miaka kadhaa sasa na wanatumai kuwafanya mapacha walioungana kuonekana kuwa ni jambo la kawaida. Wawili hao walifunguka kuwa huwa wanapata maswali mengi kuhusu jinsi ya kujamiiana na jinsi wanavyoweza kwenda bafuni na vitu kama hivyo, lakini lazima huwahimiza watu kuwa wao sio mapacha walioungana tu ila wao ni watu pia.
Kufuatia sakata hili, Ayotv imempigia Dr Maro akituelezea ni changamoto gani mapacha walioungana hupitia kwa njia za kitaalam zaidi, msikilize
TAZAMA ZAIDI;