Shirikisho la soka nchini Morocco limetangaza kuwa mapato ya mechi ya jioni ya leo ya kandanda kati ya Morocco na Burkina Faso, iliyofanyika katika mji wa Lens nchini Ufaransa, yatatolewa kwa ajili ya misaada ya tetemeko la ardhi.
Wanachama wa timu ya taifa ya kandanda ya Morocco, ambayo ilifika nusu fainali katika Kombe la Dunia la hivi majuzi nchini Qatar, walipumzika kutoka mazoezi ya Jumapili ili kuchangia damu kusaidia waathiriwa wa tetemeko.
Lakini pia wachezaji wa timu ya taifa ya kandanda ya Gambia wamechangia damu katika kituo kimoja huko Marrakesh nchini Morocco baada ya tetemeko la ardhi la kipimo cha 6.8 kupiga nchi hiyo.
Wananchi waliripoti katika hospitali za Marrakesh na kwingineko kuchangia damu kwa ajili ya majeruhi. Miongoni mwa wafadhili hao walikuwa wachezaji wa timu ya taifa ya kandanda ya Morocco.
Wafanyakazi wengine wa kujitolea walipanga chakula na bidhaa muhimu kusaidia waathiriwa wa tetemeko, baada ya malalamiko kwamba mamlaka ilichelewa kujibu.
“Kila mtu lazima ahamasishe,” alisema mfanyakazi mmoja wa kujitolea, Mohamed Belkaid, 65. “Na hiyo inajumuisha mamlaka, lakini wanaonekana kuwa hawapo.”