Mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara ambazo zilihusisha timu za Yanga na Simba,zilizochezwa hapa 88.5 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki zimeingiza jumla ya sh. 101,165,000.
Upande wa Yanga ambayo iliifunga Ruvu Shooting magoli 7-0 mechi yake peke yake iliingiza jumla ya sh. 68,450,000 kutokana na washabiki 11,972 kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Mgawo Katika mechi hiyo kila klabu ilipata sh. 15,687,488,Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa kutokana na mapato hayo ni sh. 10,441,525.42. Gharama za tiketi ni sh. 3,813,600 na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ilipata sh. 4,877,538.71. Uwanja sh. 8,129,231.19.
Gharama za mchezo zilikuwa sh. 4,877,538.71 wakati Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,438,769.36. Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) kila kimoja kilipata sh. 945,110.
Upande wa mechi ya Simba na JKT Ruvu ilishuhudia na watazamaji 5,850 na kuingiza sh. 32,715,00 kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 4,990,423.73.
Kila klabu ilipata mgawo wa sh. 7,428,742 wakati tiketi ni sh. 2,542,400 huku gharama za mechi zikiwa 2,266,395.86. Uwanja ulipata sh. 3,777,326.44 wakati Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ni sh. 2,266,395.86.
Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) ulipata mgawo wa sh. 1,133,167.93 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 881,376.17.