Wizara ya Afya ya Libya imesema mapigano yaliyotokea tarehe 15 katika mji wa Tripoli yamesababisha vifo 27 na majeruhi 106.
Wizara hiyo pia imesema familia zaidi ya mia mbili zimehamishwa kutoka kwenye maeneo yenye mapigano na vituo vitatu vya afya vimewekwa kwa ajili ya kuwaokoa majeruhi.
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya huko, mapigano hayo yalianza usiku wa tarehe 14 baada ya kamanda mmoja wa vikosi vya jeshi la serikali kukamatwa na vikosi vya ulinzi wa Rais siku chache zilizopita.
Wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo ilisema mapigano hayo yalisitishwa tarehe 15 kufuatia upatanishi.
Tazama pia…..