Umoja wa Mataifa umeripoti kuweko njaa kali ya zaidi ya Wasudan 20, huku mgogoro mkali kati ya jeshi na vikosi vya msaada wa haraka RSF ukiendelea katika maeneo mbalimbali ya Sudan.
Hivi sasa wakati wa Darfur Kusini wananyemelewa na janga kubwa zaidi la njaa.
Shirika la habari la Tasnim limenukuu taarifa ya Umoja wa Mataifa ikisema kuwa hali imeendelea kuzorota kiuchumi huku mapigano baina ya majenerali wa kijeshi yakiendelea huko Sudan.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, zaidi ya Wasudan milioni 20 na laki tatu wanapambana na njaa kali. Idadi hiyo ni takriban asilimia 42 ya wananchi wote wa Sudan, nchhi ambayo ina takriban watu milioni 45.
Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa “FAO” nchini Sudan amesema kuwa, Sudan ni moja ya nchi zenye kesi kubwa zaidi za uhaba wa chakula duniani na hali ni mbaya kiasi kwamba familia nyingi ziko kwenye matatizo na mateso yasiyofikirika.
Kwa mujibu wa gazeti la Sudan Tribune, idadi ya watu wa Sudan wanaopambana na njaa itaongezeka katika kipindi cha miezi miwili ijayo.