Nchini Ethiopia, mapigano yanaendelea kushuhudiwa katika jimbo la Tigray, lakini imekuwa ni vigumu kufahamu ni wapi yanapotokea kwa sababu ya mawasiliano mabaya.
Ikumbukwe zimepita siku 45 tangu Waziri Mkuu, Abiy Ahmed aagize operesheni ambayo ilibaini kuwa imemalizika ingawa hakuna kiongozi hata mmoja wa chama cha Tigrayan TPLF ambaye amekamatwa.
Ahmed ameendelea kutegemea kupata uugwaji mkono kutoka kwa vikosi vya Eritrea, hata kama Asmara inaendelea kukanusha kuhusika katika vita hivyo.
Aidha, anaendelea kupata msaada mkubwa kutoka kwa wanamgambo na vikosi maalum katika mkoa wa Amhara, ambao unapakana na Tigray.
WAZIRI MKUU AMTUMBUA MKANDARASI “HAIWEZEKANI, ONDOA KUBEMBELEZA SIO SERIKALI HII”