Rais wa Niger Mohamed Bazoum alisalia kuzuiliwa katika ikulu ya rais Alhamisi alasiri na haikufahamika ni nani aliyechukua mamlaka ya nchi hiyo, baada ya wanajeshi Jumatano jioni kutangaza mapinduzi ya kijeshi.
Kufuatia mapinduzi hayo, operesheni za kibinadamu za Umoja wa Mataifa nchini Niger “zimesitishwa”, msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric ametangaza siku ya Alhamisi.
Mamia kwa maelfu ya raia wamelijitokeza mitaani kuunga mkono vikosi vya ulinzi na usalama kwa mapinduzi waliofanya dhidi ya utawala wa rais Mohamed Bazoum.
Wakati huo huo msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric alitangaza siku ya Alhamisi kwamba operesheni za kibinadamu za Umoja wa Mataifa nchini Niger “zimesitishwa” Kufuatia mapinduzi hayo.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Kibinadamu (OCHA), idadi ya watu wanaohitaji msaada wa kibinadamu nchini humo imeongezeka kutoka milioni 1.9 mwaka 2017 hadi milioni 4.3 mwaka 2023, na idadi ya watu wenye uhaba mkubwa wa chakula inatarajiwa kufikia milioni 3 kati ya mwezi Juni na Agosti, kabla ya mavuno yajayo.
Washirika wa kikanda na kimataifa wa Niger wanajitahidi kujibu mapinduzi ya kijeshi ambayo wachambuzi wa kisiasa wanasema yanaweza kuwa na madhara makubwa kwa maendeleo ya kidemokrasia na mapambano dhidi ya uasi wa wanamgambo wa kijihadi katika Afrika Magharibi. Hapa ni nini kiko hatarini.