Mwezi August mwaka 2015 siku chache kabla ya dirisha la usajili la Ligi Kuu soka Tanzania bara halijafungwa, golikipa wa muda mrefu katika soka aliyewahi kucheza katika vilabu kadhaa ndani na nje ya Tanzania Ivo Mapunda alikuwa hajui hatma yake ndani ya klabu yake ya Simba, licha ya kuwa walikuwa wamempa dau la awali la usajili.
Simba walimtema Ivo Mapunda siku chache kabla ya dirisha la usajili halijafungwa, tukio ambalo lilipelekea golikipa huyo kukaa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi mitatu na kuishia kufanya mazoezi binafsi, kabla ya kuamua kuomba uongozi wa klabu ya Azam FC wampe nafasi ya kufanya mazoezi wakati akiwa anasubiri mipango yake ya kujiunga na klabu ya AFC Leopard ya Kenya ikae sawa.
“Ni kweli Ivo alikuja Azam FC na kuomba uongozi umpe nafasi ya kufanya mazoezi wakati ambao alikuwa akisubiria mipango yake ya kwenda kucheza soka nje ya nchi, lakini kilichotokea ni kuwa kocha ameonesha kuvutiwa na uwezo wake, kwa hiyo kinachoendelea sasa hivi kati ya Ivo na Azam FC ni mazungumzo ambayo yanaendelea vizuri” >>>> Jafari Iddi
November 25 uongozi wa Azam FC kupitia kwa afisa habari wake Jafari Iddi Maganga umethibitisha kocha wao mkuu wa klabu hiyo muingereza Stewart Hall kuvutiwa na uwezo wa golikipa huyo, hivyo ameomba uongozi wa Azam FC kumsajili golikipa huyo ili waongeze nguvu kikosi chao.
Hii ni sauti ya Jafari Iddi
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.