Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) imefanya ziara siku mbili ya ukaguzi katika mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) kuanzia Dar es Salaam – Dodoma (Lot1 &2), Juni 20 na 21, ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa kukagua miradi yote ya kimkakati nchini.
Akizungumza baada ya ziara hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya PPRA, Dkt. Leonada Mwagike wameona kazi nzuri iliyofanywa ambapo wamevutiwa na jinsi ambavyo kazi kubwa ya usimamizi wa kitaalam imefanywa na watanzania.
Ziara hiyo ilifanyika kwa treni kupitia njia ya Reli hiyo ya kisasa.