Jeshi la Polisi Tanzania linesema limekuwa likipokea simu nyingi kutoka kwa Waandishi wa Habari wakiuliza Polisi wamefikia hatua gani kwenye uchunguzi wa video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha tukio la Msichana aliyefanyiwa vitendo vya ukatili ambapo Jeshi hilo limesema uchunguzi unaendelea vizuri na Wananchi waendelee kuwa na subira kwani taarifa itatolewa baada ya kukamilisha yale ambayo sheria za Nchi zinavyoelekeza.
Taarifa iliyotolewa leo August 06,2024 na Msemaji wa Polisi, David Misime imesema “Pia Jeshi la Polisi linatoa wito sote kwa pamoja tuendelee kutafakari namna tunavyoendelea kujadili jambo hili na tunavyotoa maoni kwenye mitandao
ya kijamii na kwenye vyombo vya habari je hatuendelei kumtonesha huyu Binti majeraha aliyonayo moyoni?, je, kwa kuendeleza hayo Familia yake hatuendelei kuijeruhi kisaikolojia?”
“Pia tunaendelea kusisitiza mwenye taarifa ya ziada atuwasilishie kwa njia ilivosahihi kwa kutumia mifumo iliyoopo bila kuendelea kumuumiza, aidha tunaendelea kuwashukuru wale walitupatia taarifa mbalimbali huo ndiyo uzalendo wa dhati wa kuchukia vitendo vya kihalifu kama hivi”