Ni habari za Kimataifa, Moja kwa Moja kutokea Bara Ulaya ambapo mazungumzo yameanza baina ya Ukraine na Urusi ambazo zipo katika mzozo wa kivita.
Hatua hiyo inakuja ikiwa ni siku 5 baada ya Majeshi ya Urusi kuingia na kuishambulia Ukraine.
Tayari wajumbe kutoka nchi hizo mbili wameanza mazungumzo, ambapo Ofisi ya rais wa Ukraine inasema inataka kusitishwa mara moja kwa mapigano na kuondolewa kwa vikosi vya Urusi.
Wakati huo huo Msocow inataka kufikia makubaliano ambayo yalikuwa kwa maslahi ya Pande zote mbili, kulingana na mpatanishi wa Urusi, Vladimir Putin.
Kabla ya mkutano huo kuanza, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliwataka Wanajeshi wa Urusi kuweka chini silaha zao, na kutoa wito kwa EU kuipatia Ukraine uanachama wa umoja huo mara moja.
RAIS PUTIN ASIMAMISHWA KAZI, SHIRIKISHO LATOA TAARIFA “VITA, ANA MKANDA MWEUSI”