Club ya FC Barcelona ya Hispania baada ya kushindwa kutuma ofa ya maana kwa club ya Paris Saint Germain ili kumsajili Neymar, wametuma ofa ya kuomba kumsajili staa huyo kwa mkopo.
Neymar ameachwa nje ya kikosi cha PSG kwa mara ya pili sasa katika mchezo wa Ligi Kuu Ufaransa, jambo ambalo linaashiria kuwa PSG hawana mpango nae tena kutokana na staa huyo akili yake haipo PSG.
Vyanzo vya habari vinaripoti kuwa PSG wanataka pound milioni 200 ili wamuachie Neymar arudi Barcelona, dau ambalo Barcelona wanashindwa kulifikia na wanamtaka kwa mkopo wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kumchukua jumla.
Mpango wa Neymar kuondoka PSG linaweza kutimia kutokana na Barcelona na Real Madrid kumuwania staa huyo, mkurugenzi wa michezo wa Barcelona Eric Abidal na mwanachama ya wa bodi Javier Bordas walikuwa Paris wiki iliyopita kwa ajili ya mazungumzo na PSG ila hawajafikia muafaka, inaaminika kabla ya dirisha la usajili kufungwa Ulaya September 2 Neymar atakuwa kaondoka PSG.