Wakati wabunge wakiendelea kuijadili bajeti kuu ya serikali trilion 29.5, Mbunge wa Korogwe vijijini Stephen Ngonyani maarufu kama Maji marefu amesimama bungeni kuhoji sababu za serikali kusahau kuongelea suala la sukari katika bajeti yake.
Maji marefu amesema…>>>’Mmeacha bei ya petrol kama ilivyo, ningeomba mpandishe. Maana ya kupunguza bei ya mafuta inamaana wasafiri wapunguziwe gharama lakini hakuna mtanzania yeyote ambaye amepunguziwa gharama za nauli‘
‘Kwasababu hatufaidiki kwa lolote ningeomba mpandishe petrol mtupunguzie sukari, sukari hamjaiongelea hapa lakini sukari ni kitu muhimu sana kwa Watanzania‘- Mbunge Maji marefu
ULIIKOSA HII? YA KANGI LUGOLA KWA WAZIRI WA FEDHA KWENYE UTUMBUAJI MAJIPU
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE