Marais wastaafu wa Marekani, Barack Obama, George Bush na Bill Clinton wamejitolea kupewa chanjo ya ugonjwa wa corona kwa uwazi.
Viongozi hao ambao wawili ni Wanachama wa Chama cha Democrat na mmoja wa Republican wamesema watapata chanjo hiyo punde tu itakapoidhinishwa na wadhibiti wa maafisa wa afya.
Hatua hiyo inakusudiwa kuimarisha imani ya raia juu ya usalama na ufanisi wa chanjo za virusi vya corona.
Kura za maoni zinaonesha kuwa idadi kubwa ya watu hawana haraka ya kupata chanjo hiyo.
Hadi kufikia sasa hakuna chanjo ambayo imeidhinishwa na Marekani lakini wadhibiti wa serikali wanaanza kufuatilia chanjo ya kampuni za kampuni za Pfizer na Moderna wiki zijazo.
“Nawaahidi itakapoanza kupatikana kwa watu walio katika hatari kubwa, nitaipata,” amesema Obama.