Rais wa Marekani Joe Biden ameahidi siku ya Jumapili (Oktoba 1) kwamba Marekani haitaitelekeza Ukraine iliyokumbwa na vita, baada ya makubaliano ya kuzuia kuzorota kwa serikali ya shirikisho kuacha msaada wa ziada kwa Kiev.
“Ninataka kuwaambia washirika wetu, kwa raia wa Marekani na raia wa Ukraine, mnaweza kutegemea msaada wetu. Hatutaitenga” Ukraine, amesema katika hotuba yake kwenye televisheni.
Kwa upande wake, Kyiv imetangaza Jumapili kwamba “inafanya kazi” na Marekani. “Serikali ya Ukraine inafanya kazi kikamilifu na mshirika wake, Marekani, ili kuhakikisha kuwa uamuzi mpya wa bajeti ya Marekani utajumuisha ufadhili mpya wa kuisaidia Ukraine,” amesema msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Oleg Nikolenko.
Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Rustem Umerov amesema kwenye mtandao wa kijamii Jumapili kwamba alikuwa amezungumza na mwenzake wa Marekani, Lloyd Austin, kujadili kuendelea kwa msaada wa kijeshi wa Marekani. Marekani imeisaidia zaidi Kyiv, ikitoa msaada wa kiraia na kijeshi wa dola bilioni 110 tangu mwrzi Februari 2022.