Marekani imesema imetoa mapipa Milioni 30 ya mafuta kutoka kwenye hifadhi yake ya kimkakati ya mafuta huu ukiwa ni sehemu ya mpango wa muungano wa Nchi 30 ambazo zimekubaliana kutoa mapipa Milioni 60 ya mafuta kutoka kwenye hifadhi zake kote ulimwenguni ili kukabiliana na kupanda kwa bei ya mafuta Duniani kulikochangiwa na mzozo wa Ukraine na Urusi.
Marekani imesema “Tuko tayari kufanya zaidi ikibidi, tukiwa na umoja na washirika wetu, hatua hizi zitasaidia bei butu ya gesi hapa nyumbani na najua habari kuhusu kinachoendelea inaweza kuonekana kuwa ya kutisha lakini nataka mjue kuwa tutakuwa sawa”
Wiki iliyopita bei ya mafuta ilipanda na kuvuka dola mia moja kwa mara ya kwanza tangu miaka saba iliyopita ambapo ongezeko hili linatajwa kusababishwa na hofu juu ya ugavi baada ya Mzalishaji mkubwa wa mafuta Urusi kufanya mashambulio nchini Ukraine.
Bei ya mafuta ghafi kwenye Bara la Ulaya sasa imefikia dola 105 na senti 79 kwa pipa, inafahamika kwenye Nchi zinazozalisha mafuta duniani Urusi ni Mzalishaji muhimu baada ya Saudi Arabia miongoni mwa nchi za shirika la wauzaji mafuta la OPEC.
FAHAMU MATAIFA TISA YENYE UWEZO MKUBWA WA SILAHA ZA NYUKLIA DUNIANI, URUSI KINARA
VITA IMEANZA: TAZAMA KOMBORA LILIVYOTUA KATIKATI YA MJI WA UKRAINE “SHAMBULIO BAYA”