Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya Urusi ili kujibu kile inachosema ni mashambulio ya kimtandao na matendo mengine ya uadui.
Hatua hizo, ambazo zinawalenga maafisa na taasisi, zinanuia kuzuia shughuli za madhara za “Urusi katika mataifa ya kigeni “, ilisema White House.
Taarifa ilisema kuwa idara ya ujasusi ya Urusi ilikuwa nyuma ya udukuzi mkubwa uliofanyika katika “SolarWinds”, na ikaishutumu Moscow kuingilia katika uchaguzi wa mwaka 2020.
Muda mfupi baada ya vikwazo kutangazwa, Wizara ya mambo ya nje ya urusi iliviita “hatua za uadui ambazo zinaibua joto la malumbano “.