Rais Joe Biden alisema siku ya Jumatano aliiomba Wizara ya Ulinzi ya Marekani kuendelea kupeleka silaha nchini Ukraine baada ya kulaani shambulizi la Urusi siku ya Krismasi dhidi ya baadhi ya miji ya Ukraine na mfumo wake wa nishati.
“Madhumuni ya shambulio hili la kutisha lilikuwa kuwakatisha watu wa Ukraine ufikiaji wa joto na umeme wakati wa msimu wa baridi na kuhatarisha usalama wa gridi yake,” Biden alisema katika taarifa.
Rais mteule wa chama cha Republican Donald Trump atachukua nafasi ya Democrat Biden mnamo Januari 20.
Urusi ilishambulia mfumo wa nishati wa Ukraine na baadhi ya miji kwa makombora ya cruise na balestiki pamoja na ndege zisizo na rubani siku ya Jumatano, Ukraine ilisema. Tangu Urusi ilipovamia Ukraine kikamilifu mwaka 2022, Washington imetoa msaada wa dola bilioni 175 kwa Ukraine