Rais Donald Trump alitangaza Jumatatu kuwa anaiondoa Marekani kutoka kwenye Shirika la Afya Ulimwenguni, katika hatua kubwa ambayo ilisababisha ukosoaji mkubwa kutoka kwa wataalam wa afya ya umma katika siku yake ya kwanza kurudi Ikulu.
Trump amekuwa akilikosoa shirika la afya la Umoja wa Mataifa kwa muda mrefu, na utawala wake ulianza rasmi kujiondoa kutoka WHO mnamo Julai 2020 huku janga la Covid-19 likiendelea kuenea.
Kwa mujibu wa shirika la habari la CNN miaka minne iliyopita, Rais wa wakati huo Joe Biden alisitisha kuondoka kwa Marekani kutoka kwenye bodi iliyopewa jukumu la kuratibu mwitikio wa kimataifa wa dharura za kiafya katika moja ya hatua zake za kwanza baada ya kuchukua Ikulu ya White House.
Maandishi ya agizo kuu la Jumatatu yanataja “shirika lisiloshughulikia janga la COVID-19 ambalo liliibuka kutoka Wuhan, Uchina, na majanga mengine ya kiafya ya ulimwengu, kushindwa kwake kupitisha mageuzi yanayohitajika haraka, na kutokuwa na uwezo wa kuonyesha uhuru kutoka kwa ushawishi usiofaa wa kisiasaya nchi wanachama wa WHO,” kama sababu za kujiondoa kwa Marekani.
“Hilo ni jambo kubwa,” Trump alimwambia msaidizi wakati akianza kutia saini amri ya utendaji, akiashiria uamuzi wake wa 2020 na imani yake kwamba Marekani ilikuwa inalipa fedha nyingi kwa shirika ikilinganishwa na nchi nyingine. Mnamo 2020, Trump pia alishutumu shirika hilo kwa kusaidia Uchina kwa madai ya kuficha asili ya Covid-19 na kuruhusu kuenea kwake.