Mwanasheria Mkuu wa Marekani, William Barr amewaamuru waendesha mashtaka wa Serikali kuanzisha uchunguzi kuhusu dosari katika upigaji kura.
Ameagiza hilo baada ya Rais Donald Trump kudai kuwa alishindwa kutokana na udanganyifu. Barr amesema Wizara ya Sheria haina ushahidi wa matukio ya udanganyifu.
Uchunguzi wa udanganyifu katika upigaji kura kawaida hufanywa na Majimbo binafsi, ambayo huweka na kuchunguza kanuni zao za Uchaguzi.
Amri ya Barr imekuja wakati Trump akipambana kuubatilisha ushindi wa mpinzani wake kutoka Democratic, Joe Biden katika Majimbo 4 muhimu.