Mamlaka nchini Marekani zinasema wana imani kuwa wataweza kukabiliana na vitisho vyoyote vya usalama kuelekea uchaguzi wa rais mwezi Novemba.
Huko Alexandria, Virginia, Mwandishi wa VOA, Veronica Balderas Iglesias alihudhuria mafunzo ya maafisa wa uchaguzi, moja ya hatua kadhaa za kuhakikisha upigaji kura huru, wa haki na wazi.
Mwezi uliopita, maafisa wa juu wa Marekani waliliambia Bunge kuwa uchaguzi wa Rais wa Marekani utakuwa wa haki na salama, shukran kwa kuimarisha ulinzi na kuongeza ushirikiano kati ya serikali kuu, mamlaka za majimbo na serikali za wilaya.
Jen Easterly, Mkuruguenzi wa Shirika la Usalama wa Mitandao na Miundombinu ya Kiusalama, kaskazini mashariki Washington, amesema: “Kuanzia uhalifu wa mitandao, mpaka vitisho vya kimwili, hatari za uendeshaji, na kutoka kwa ushawishi mbaya wa kigeni. Jombo moja la kuangalia, hapo kuna utofauti katika miundo mbinu ya uchaguzi wetu, kwasababu unashughulikiwa na serikali, na mamlaka 8,800 tofauti kote nchini, kwahiyo utofauti unaipa uthabiti.