Msemaji wa shirika hilo ameeleza katika taarifa, kwamba USAID na serikali ya Ethiopia wamegundua kuwapo kwa hila iliyoratibiwa, ya kuubadishia njia msaada wa chakula ili usiwafikie wenye mahitaji. Ingawa msemaji huyo hakuwataja wahusika, nyaraka za muungano wa mashirika ya msaada zinawatuhumu maafisa wa tawala za mikoa na vikosi vya jeshi kujinufaisha na msaada huo.
Marekani ndiyo mfadhili mkubwa kabisa wa Ethiopia katika sekta ya msaada wa kibinadamu, ambapo inawasaidia watu wapatao milioni 20 wanaokumbwa na njaa kutokana na ukame na pia vita katika jimbo la Tigray ambavyo vilimalizika hivi karibuni.
Marekani ndiyo mfadhili mkubwa zaidi wa kibinadamu kwa Ethiopia, ambapo zaidi ya watu milioni 20 wanahitaji msaada wa chakula, wengi wao kutokana na ukame na vita vilivyohitimishwa hivi karibuni katika eneo la kaskazini la Tigray.
Kulingana na taarifa ya ndani ya kundi la wafadhili wa kigeni kwa Ethiopia iliyoonekana na Reuters, USAID inaamini kuwa chakula hicho kimeelekezwa kwa vitengo vya kijeshi vya Ethiopia.
USAID na Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) tayari walikuwa wamesitisha msaada wa chakula kwa eneo la kaskazini mwa Ethiopia la Tigray mwezi uliopita kutokana na taarifa kwamba kiasi kikubwa cha misaada kilikuwa kinaelekezwa kinyume.
Vita vya miaka miwili huko Tigray kati ya serikali ya shirikisho na vikosi vinavyoongozwa na chama kikuu cha kisiasa katika eneo hilo vilimalizika kwa mapatano mnamo Novemba baada ya kuua makumi ya maelfu ya watu na kusababisha hali kama ya njaa kwa mamia kwa maelfu.