Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani alisema jana Jumatatu kabla ya kufanyika mazungumzo kati ya Rais Vladimir Putin wa Russia na Kim Jong Un Kiongozi wa Korea ya Kaskazini kuwa Washington haitasita kuziwekea vikwazo nchi hizo mbili.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Irna, Mitthew Miller Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani amebainisha mbele ya waandishi wa habari kuwa kutumwa silaha za Korea Kaskazini nchini Russia kunakiuka maamizio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kwamba nchi yake haitasita kuziwekea vikwazo vipya Moscow na Pyongyang.
Kabla ya kutangaza Korea Kaskazini na Russia uamuzi wa Kim Jong kuitembela Russia kwa mwaliko wa Rais Putin, White House ilimtaka Kim Jong asikabidhi au kuiuzia Moscow silaha zake.
Huku akitangaza kukutana viongozi wawili wa Korea Kaskazini na Russia mjini Moscow, Dmitry Peskov Msemaji wa Kremlin ameongeza kuwa mazungumzo hayo yatakuwa marefu. Pamoja na kuashiria kufanyika mazungumzo hayo karibuni, Peskov amesema uhusiano wa pande mbili utapewa kipaumbele muhimu.