Imetajwa kuwa kiwango cha ukuaji duniani kote mwaka uliopita ulikuwa chini ya asilimia moja na Marekani imeongeza watu milioni 1.7
Idadi ya watu duniani imeongezeka kwa milioni 75 katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita na siku ya mwaka mpya itafikia zaidi ya watu bilioni 8 kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Ofisi ya Hesabu ya watu Marekani siku ya Alhamisi.
Kiwango cha ukuaji duniani kote mwaka uliopita ulikuwa chini ya asilimia moja. Mwanzoni mwa mwaka 2024 watoto wanaozaliwa 4.3 na vifo viwili vinatarajiwa duniani kote kila sekunde kwa mujibu wa takwimu za sensa.
Kiwango cha ukuaji wa Marekani katika mwaka uliopita kilikuwa asilimia 0.53 karibu nusu ya takwimu ya kimataifa.
Marekani imeongeza watu milioni 1.7 na itakuwa na idadi ya watu katika siku ya mwaka mpya kwa watu milioni 335.8.
Kama kasi ya sasa itaendelea hadi mwisho wa muongo basi miaka ya 2020 inaweza kuwa muongo wenye kasi ya polepole zaidi ya ukuaji katika historia ya Marekani na kueka kiwango cha ukuaji wa idadi ya watu chini ya asilimia 4 kwa kipindi cha 2020 hadi 2030 alisema William Frey, mtaalamu wa masuala ya takwimu katika Taasisi ya Brookings.
Muongo unaokua polepole zaidi sasa ulikuwa baada ya hali mbaya sana ya uchumi-Great Depression katika miaka ya 1930 wakati kiwango cha ukuaji kilikuwa asilimia 7.3.