Msanii Marioo kutoka Tanzania kwa kushirikiana na msanii Ahmed Gamal kutoka Misri wametengeneza wimbo wa pamoja kwa ajili ya Bwawa Letu La Nyerere.
Wimbo huo ambao umeimbwa leo mbele ya Rais Dkt Samia Suluhu unaeleza tumaini la Tanzania katika bwawa hilo, na kuonesha namna ambavyo Watanzania wanajivunia kwa kuwa mradi huo mkubwa unatekelezwa kwa fedha za Watanzania kwa faida ya Watanzania.