Mwanamuziki nyota wa Bongo Flava, Omary Ally Mwanga, anayefahamika kwa jina la kisanii Marioo, ametambulishwa rasmi kama Balozi wa Bahati Nasibu ya Taifa ya Tanzania. Ushirikiano huu wa kimkakati unaleta matumaini, burudani, na fursa zinazoweza kubadilisha maisha ya Watanzania.
Huku Bahati Nasibu ya Taifa ikikaribia kuzinduliwa rasmi, Kampuni ya ITHUBA, ambayeni mwendeshaji rasmi aliyepewa dhamana ya miaka nane, inaleta enzi mpya ya ushindi ambapo kuamini katika uwezekano wa kitu kunageuza ndoto kuwa uhalisia.
Katika kiini cha bahati nasibu hii ni kauli mbiu yenye nguvu: “Amini. Cheza. Ushinde.”
Huu sio msemo wa kawaida—bali ni mwamko wa kuhamasisha Watanzania kuota ndoto kubwa, kuthubutu, na kuchukua hatua za kuyafikia mafanikio.
Akizungumzia jukumu lake jipya kama balozi wa Bahati Nasibu ya Taifa, Marioo hakuweza kuficha furaha yake:
“Nina furaha kubwa kutangaza kuwa mimi sasa ni balozi rasmi wa Bahati Nasibu ya Taifa! Huu ni wakati mkubwa—sio tu kwangu kama msanii, bali kwa kila Mtanzania anayethubutu kuota ndoto kubwa. Bahati Nasibu ipo hapa kufungua milango, kutengeneza washindi, na kuinua jamii—nami najivunia kuwa sehemu ya safari hii!”
Ushirikiano huu unamaanisha kwamba ushindi si ndoto tena—bali ni uhalisia unaosubiri kutokea!
Mkurugenzi kutoka ITHUBA Tanzania, Kelvin Koka, alisisitiza kuwa ushawishi wa Marioo unamfanya kuwa kiungo bora kati ya burudani na michezo ya kubahatisha.
“Marioo ni zaidi ya msanii—yeye ni alama ya kizazi kipya cha Watanzania wanaothubutu kuamini katika ndoto zao. Nguvu yake, uhalisia wake, na uhusiano wake wa karibu na mashabiki wake vinamfanya kuwa balozi sahihi wa Bahati Nasibu ya Taifa. Kupitia yeye, tutahamasisha Watanzania wengi zaidi kushiriki kwenye michezo ya bahati nasibu ambayo ni ya haki, ya kusisimua, na yenye uwezo wa kubadilisha maisha,” alisema Koka.
Lakini Bahati Nasibu ya Taifa haihusiani tu na ushindi binafsi—ni chombo cha maendeleo kinachowekeza katika miradi ya michezo ili kuinua vipaji na kusaidia jamii.
“Tumejidhatiti katika uwazi, ubunifu, na michezo inayowajibika. Kila tiketi inayouzwa inachangia maendeleo ya taifa, kuhakikisha kuwa washindi si watu binafsi pekee bali ni Watanzania wote kwa ujumla,” aliongeza Koka.
Ushirikiano wa Marioo unazinduliwa kwa kampeni kubwa za kitaifa, matukio ya kusisimua, na jackpots za kiwango cha juu ambazo zitawageuza mashabiki wake kuwa washindi.
“Mengi mazuri yanakuja! Kuna jackpots kubwa, matukio makubwa, na fursa kwa mashabiki wangu kushinda kama hawajawahi kushinda kabla. Hii ni mwanzo tu—Tanzania, jiandaeni!” Marioo alidokeza.
Muda wa kusubiri umekwisha. ITHUBA Tanzania iko tayari kuandika historia—ikibadilisha kila siku ya kawaida kuwa siku ya ushindi kwa kila Mtanzania!
Kwa kutumia hashtag rasmi #BahatiNasibuYaTaifa na #Inakuja, Bahati Nasibu ya Taifa inalenga kuongeza ushiriki wa kidijitali na kuwahamasisha Watanzania kote nchini kushiriki.