Chama cha soka Ubelgiji kimetangaza kuwa Kocha Mkuu wa Ubelgiji Roberto Martinez hatoendelea tena na timu hiyo.
Maamuzi hayo ya Martinez hayajafanyika leo baada ya kuondolewa Kombe la Dunia bali tayari yakikuwa yameshafanyika kabla ya mashindano.
Ubelgiji leo wameaga Kombe la Dunia baada ya sare ya 0-0 dhidi ya Croatia na kuwafanya wanalize nafasi ya tatu wakiwa na alama 4, Croatia nafasi ya pili alama 5 na Morocco nafasi ya kwanza akiwa na alama 7.