Jeshi la Polisi kikosi cha Bohari kuu imepiga marufuku kwa mafundi wa kushona mitaani kutojiusisha na ushonaji wa sare za Polisi kwani kufanya hivyo ni kosa ma hatua kali za kisheria zita hukuliwa juu yao.
Hayo yamesemwa na Inspector Leokardia akiongea katika mahojiano maalum na AyoTV na kusisitiza kumekua na tabia ya baadhi ya Mafundi mitaani kuwashonea askari sare polisi na mda mwingine ushona sare na kuwapa wahalifu kwenda kutenda uhalifu sasa hilo ni kosa kubwa mwenye wajibu wa kuwashonea askari zao ni bohari kuu ya polisi tu na si mtu mwingine hivyo na askari wanajua hilo.
“Kikosi cha Bohari ndio kinasimamia ushonaji ili kudhibiti ushonaji holela naoweza kupatikana mitaani,mtu yeyote anayeshona mtaani ni kosa la jinai na ukipatikana unashona tutakufikisha mahakamani”